SMZ NA SMT KUTOA ELIMU YA MUUNGANO KWA WANANCHI.
Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Sera Uratibu Na Baraza La Wawakilishi Mhe Hamza Hassan Juma Amesema Muungano Wa Tanganyika Na Zanzibar Ndio Tunu Pekee Ya Watanzania Inayowaweka Pamoja Katika Kuimarisha Maendeleo.
Akizungumza Katika Kikao Cha Ushirikiano Baina Ya Ofisi Ya Makamu Wa Pili Wa Rais Zanzibar Na Ofisi Ya Makamu Wa Rais Tanzania Kwa Ajili Ya Kujadili Masuala Ya Muungano Na Yasiyo Ya Muungano Waziri Hamza Amesema Watanzania Wanapaswa Kuutumia Muungano Kama Ni Fursa Katika Kukuza Uchumi Ujamaa Na Ulinzi Kwa Kupitia Sekta Mbalimbali Ikiwemo Michezo.
