RAIS SAMIA AZINDUA SAFARI YA TRENI YA SGR KUTOKA DAR ES SALAAM HADI DODOMA

Kiasi cha fedha Shilingi Trilioni 10 zimetumika katika ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR )kwa vipande vya kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma ikiwa dhamira ya Serikali ni kutanua Wigo wa kibiashara ambapo Reli hiyo inatarajiwa  kufika hadi Nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

RAIS SAMIA AMEIAGIZA WIZARA YA AFYA KUKAMILILISHA UTAFITI WA KITAIFA

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Afya kukamililisha utafiti wa Kitaifa utakaobainisha hali halisi ya Wataalamu wa Afya Nchini waliopo kwenye Soko la Ajira, mahitaji na namna bora itakayoiwezesha serikali kutatua tatizo la kuajiri katika sekta hiyo.

UCHUMI WA TANZANIA UMEENDELEA KUKUA KWA ASILIMIA TANO NUKTA MBILI

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesetoa wito kwa Wadau wa Sekta Binafsi kushirikiana Serikali kuekeza katika Miradi ya ubia kati ya Sekta ya umma na Binafsi hapa Nchini

Miradi hiyo ni pamoja na kutengeza Vifaa vya Ujenzi Miundombinu ya Barabara za Tozo na Ujenzi wa maeneo maalum ya Viwanda .

RAIS SAMIA AMUAGA RAIS WA MSUMBIJI.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan  akimuaga Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abedi amani.

Katika Uwanja wa Ndege Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wamehudhulia kumuaga Rais Nyusi.

Vikundi mbali mbali vya Utamaduni vimetumbuiza katika kumuaga Rais huyo.

RAIS SAMIA AMEAGIZA KUSAJILIWA TAASISI ZOTE ZA UKUSANYAJI WA TAARIFA ZA WATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka tume ya Ulinzi wa taarifa Binafsi Tanzania (PDPC) kuhakikisha ifikapo Disemba Mwaka huu iwe imezisajili Taasisi zote za Umma na Binafsi zinazohusika na ukusanyaji na uchakataji wa Taarifa na kuzisimamia kwenye kutekeleza sheria ya ulinzi wa Taarifa Binafsi. 

VIONGOZI WA CCM WAMETAKIWA KUACHA KUHUJUMIANA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka Viongozi wa Chama hasa wa  Matawi kuwashawishi Vijana kujiunga na CCM  ili kiweze kupata Wanachama wengi na kukiwezesha kushinda katika uchaguzi wa Mwaka 2025.

NCHI INAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA IKIWA NI MIONGONI MWA DHAMIRA YA MAPINDUZI YA MWAKA 1964.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Nchi inaendelea kuimarisha huduma za afya ikiwa ni miongoni mwa dhamira ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Akizungumza wakati alipozinduwa Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi huko Lumumbakatika shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Samia amesema kwa vile Hospitali hiyo itatoa huduma bora na za kisasa ni vyema watendaji na wahusika wa hospitali kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa Wananchi zinaimarika kuwa bora zaidi.

Subscribe to DKT SAMIA SULUHU HASSAN
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.