WATANZANIA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VISIVO NA MAADILI.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kujiepusha na Vitendo vinavyoenda tofauti na Mila na Desturi za Tanzania na kuendelea kulinda Amani na utulivu uliopo Nchini.

Waziri mkuu Majaliwa maetoa Kauli hiyo kwenye Baraza la Eid El Adh’haa Kitaifa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed Vi Makamo Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Jijini Dar es salaam mara baada ya kukamilika kwa swala Sikukuu ya Eid El Adh’haa.

SMT KUFANYA TATHIMINI YA UHARIBIFU WA BARABARA NA MADARAJA.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa sasa imesitisha Ujenzi wa Barabara mpya mpaka itakapokamilisha kufanya tathimini ya uharibifu wa Barabara na Madaraja uliosababishwa na Mvua zilizonyesha na badala yake kuendelea kurejesha Mawasiliano maeneo yaliyokatika.

WATENDAJI WIZARA YA MADINI KUFIKA TARIME VIJIJINI KUTATUA TATIZO LA FIDIA

Waziri Mkuu wa Tanzania amewagiza Watendaji wa Wizara ya Madini kufika Wilaya ya Tarime Vijijini  kuzungumza na Wananchi ili kutatua tatizo la fidia ambalo linawasumbua kwa muda mrefu na kuonekana wao Wakimbizi katika  ardhi yao.

Akizungumuza na Wananchi katika eneo la Nyamwaga baada ya kusikiliza  Kero hizo kutoka kwa  Wananchi waliokuwa wakizungumzia suala la fidia zinatolewa na Mgodi wa Barick North Mara.

Subscribe to MHE KASSIM MAJALIWA
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.