ZRA YAPELEKA FARAJA KWA WATU WENYE MAZINGIRA MAGUMU

    Mamalaka ya Mapato Zanzibar ZRA, imesema itaendelea kusaidia Watu wenye mazingira magumu na wenye Ulemavu ili kujiona wanathamani ndani ya Jamii.

     Akizungumza mara baada ya kugawa sadaka kwa Familia 300 ikiwemo Watu wenye mazingira magumu, Watoto wenye Ulemavu na Watu wasiojiweza, huko Bumbwini na Jangombe,  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamalaka hiyo, Profesa Hemed Rashid Hikman.

ZRA WAWATAKA WAFANYABIASHARA KUFUATA SHERIA

    Wafanyabiashara wanaosafirisha na kuingiza mizigo Zanzibar kutoka Nje ya Nchi wameshauriwa  kufanya Biashara hiyo kwa kuzingatia sheria

    Akikagua Wafanyabiashara wanauza Biashara zao kwa kuingiza  kutoka Nje Kamishna Mkuu ZRA Ndg. Yussuf Juma Mwenda amesema kumekuwa na taratibu za sheria zinakiukwa na baadhi ya Wafanyabiashara kupata hasara kwa kukosa kutoa malalamiko yao wakati wa marejesho ZRA.

WAFANYAKAZI ZRA WAPEWA MAFUNZO

    Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar kwa Pemba wametakiwa kufuata kanuni za Utumishi wa Umma pamoja na maadili ya kazi zao ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi.  

   Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na utawala ZRA Ndg.Seif  Suleiman Ali katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ZRA Pemba huko Ofisini kwao Gombani Chake Chake.

    Amesema Mafunzo hayo yamelenga kuongeza ufanisi kwa Watendaji hao na kuweza kuwahudumia walipa kodi kwa ufanisi.

ZRA KUWATAKA MAWAKALA KUSIMAMIA ULIPAJI WA KODI

     Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ZRA Ndg. Yussuf Juma Mwenda amewataka Mawakala walioruhusiwa kuingiza vileo Zanzibar kuhakikisha wanasimamia ulipaji wa kodi kikamilifu.

    Akizungumza na Mawalaka hao Kamishna Mwenda amesema kuwa wanawajibu wa kuhakikisha Mapato ya Serikali yanapatikana na kuongezeka.

    Amewahakikishia kuwa Mamlaka ya Mapato itafanya kila juhudi kuona kuwa Mawakala hao wanatekeleza vyema majukumu yao ili Serikali iendelee kupata Mapato.

Subscribe to #ZRA
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.