ZURA KUTOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA KANUNI ZA UTOAJI VIBALI KWA MAFUNDI UMEME.
Mamlaka ya kudhibiti huduma za Maji Nishati (Zura) imeshauriwa kutoa ELimu kwa Watumiaji wa Kanuni ya utoaji vibali kwa Mafundi Umeme umuhimu wa kuwepo Kanuni hiyo na utekelezaji wake.
Ikipopokea maoni ya Watumiaji wa Kanuni hiyo katika kamati ya Kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza la Wawakilishi chini ya kaimu Mwenyekiti Mhe.Mwanaasha Khamis Juma huko Maisara imebaini kuwa baadhi ya Watumiaji wa kanuni hiyo hawana uelewa kuwa tayari kanuni hiyo imeanza kutumika na kusababisha kuwepo kwa mapungufu katika utekelezaji wake.