Kauli Hiyo Imetolewa Na Kamati Ya Kuchunguza Na Kudhibiti Hesabu Za Serikali PAC, Wakati Walipokua Wakipokea Majibu Ya Hoja Zilizotolewa Na Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali, Zinazohusu Dosari Zilizojitokeza Katika Mradi Wa Ujenzi Wa Vyumba Vya Kusomea Katika Chuo Cha Kiislamu Micheweni Pemba.
Wamesema Kamati Imebaini Katika Miradi Mingi Inayotekelezwa Zipo Taasisi Zinashindwa Kuonesha Hati Za Makubaliano Pamoja Na Zile Za Malipo, Ili Kuweza Kuthibitisha Uhalali Wa Malipo Yanayofanyika Katika Miradi Yao Jambo Ambalo Linapelekea Kutokuthibitika Kisheria Matumizi Hayo, Na Kupelekea Uwezekano Wa Upotevu Wa Fedha Za Serikali Ambapo Pia Ni Kwenda Kinyume Na Sheria Nambari 12 Ya Usimamizi Wa Fedha Za Umma Ya Mwaka 2016.
Nao Viongozi Wa Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar, Wamekiri Kuwepo Kwa Kasoro Hizo Na Kuahidi Kuzitafutia Ufumbuzi Wa Haraka Ili Kuweza Kuondoa Uwezekano Wa Kujirudia Mapungufu Yanayojitokeza Katika Ukaguzi.