Wito Huo Umetolewa Na Mwenyekiti Wa Kamati Ya Viongozi Wakuu Wa Kitaifa Ya Baraza La Wawakilishi Mhe. Machano Othman Said, Huko Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashtaka Chake Chake Katika Kikao Cha Uwasilishwaji Wa Tarifa Za Utekelezaji Wa Ofisi Ya Rais Katiba Sheria Na Utumishi Wa Umma Katika Kipindi Cha Robo Mwaka.
Amesema Wizara Hiyo Ndio Yenye Jukumu Kubwa La Kuhakikisha Inasimamia Haki Za Wananchi Kwa Kupata Haki Zao Na Kuilinda Serekali Katika Kuwahudumia Wananchi Hivyo Ni Vyema Kutoa Haki Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria.
Akiwasilisha Tarifa Ya Utekelezaji Wa Kipindi Cha Robo Mwaka Kaimu Mwanasheria Dhamana Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashataka Mkoa Kusini Pemba, Seif Mohamed Khamis Amesema Ofisi Imepokea Jumla Ya Majalada Ya Uchuguzi 282 Kutoka Jeshi La Polisi ZAEKA Na Mamlaka Ya Kupambana Na Madawa Ya Kulevya.
Wakichangia Katika Kikao Hicho Wajumbe Wa Kamati Hiyo Wamezitaka Tasisi Za Haki Jinai Za Wizara Hiyo Kuengeza Mashirikiano Na Kasi Ya Kuwafikia Mashahidi Ili Kutoa Haki Kwa Wakati.
Akiswasilisha Tarifa Ya Wizara Kwa Ujumla Afisa Mdhamini Ofisi Ya Rais Katiba Sheria Na Utumishi Wa Umma, Halima Khamis Ali Amesema Wizara Licha Ya Mafanikio Ambayo Wameyapata, Lakini Bado Wanakumbwa Na Changamoto Ya Ufinyu Wa Ofisi Na Uchakavu Wa Majengo.