Meneja Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba Ahmed Ali amesema Kikosi chao kiko vyema kuwakabili Al-ahly ya Misri licha ya kupoteza Mchezo wao wa Awali.
Ahmed amesema wamefanya Mazoezi yao ya Mwisho kuelekea Mchezo huo na hawana wasi wasi juu ya kupindua meza na kutinga Nusu Fainali.
Aidha Ahmed amesema haitakuwa rahisi kupata Matokeo lakini wamejipanga vyema na wako tayari kupambana.
Simba wanatarajiwa kushuka Dimbani Leo Dhidi ya Al ahly, Saa Tano Usiku huku Yanga wakishuka Dimbani dhidi ya Mamelodi, Saa Tatu Usiku
hot
standard