SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA AFYA

MKUU WA BOHARI YA DAWA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania MSD Mavere Tukai amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya Afya Nchini umechangia kuimarika kwa upatikanaji wa huduma na Bidhaa za afya.

Mkurugenzi Tukai amebainisha hayo wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari baada ya kukamilika kwa Ziara ya Wahariri ya kutembelea Ghala la MSD Kanda ya Dodoma.

Ameyataja baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na MSD kuwa ni pamoja na kufikisha Bidhaa za Afya kwa Wateja kwa zaidi ya Aslimia 84, kuongezeka kwa mzunguko wa Bidhaa za Afya na Vifaa Tiba, kufanya vizuri katika Ununuzi wa Vifaa vya Tiba ya afya ya Meno, ongezeko la Wateja kwa Aslimia 7 na ongezeko la Vituo zaidi ya 600, pamoja na mabadiliko ya MSD kiutendaji. 

Amebainisha kuwa licha ya mafanikio yaliyofikiwa lengo la MSD ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma wakati wote.

Awali Meneja wa Kanda MSD Dodoma Mwanashehe Jumaa ameeleza namana Mfumo wa usambazaji wa dawa na Vifaa tiba unavyofanya kazi.

Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari wapo katika Ziara ya Siku mbili ambapo hapo jana walitembelea Kiwanda cha kuzalisha Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe na kujionea namna Kiwanda hicho kinavyofanya kazi na leo kutembelea Ghala la MSD Kanda ya Dodoma.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.