SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YATHAMIN MICHANGO YA WAZEE

Wazee

   Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inathamini michango inayotolewa na Wazee  katika harakati za maendeleo ya  Zanzibar.

   Akizungumza kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi  na Utawala bora Mhe.Haroun Ali Suleiman  katika Ugawaji wa Sadaka amesema ni vyema kuwathamini Wazee ambao wametoa mchango katika Serikali hivyo

   Sadaka hiyo imekusudiwa Makundi mbalimbali ya Wazee kwa lengo la Kukumbuka na Kuenzi michango yao walipoitumikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

   Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu  Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema Wazee ni Hazina ya Nchi hivyo kuna kila sababu ya kuwatunza na Kuwaenzi.

   Wazee waliopatiwa Sadaka hiyo wamefurahishwa na jitihada za Rais wa Zanzibar katika kuwakumbuka hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Iddl Adh-hah.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.