SERIKALI KUGHARAMIA MASHABIKI YANGA KWENDA KWA MADIBA

Club ya Yanga

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunga Mkono Sekta ya Michezo kwa kugharamia Safari ya kuwasafirisha Mashabiki wa Timu ya Yanga kwa ajili ya Kwenda Nchini South Afrika katika Mechi ya Marudiano na Mamelod  Sundown.

     Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Khamis Mohamed Mwinjuma kwenye ghafla ya kuwaaga Mashabiki na Viongozi wa Timu hiyo kuelekea Nchini South Afrika iliyofanyika Makao Makuu ya Klabu hiyo Jijini Dar es salaam.

    Mheshimiwa Khamis Mwinjuma ameongeza kwa kuwataka Mashabiki na Uongozi wa Timu ya Yanga wakaliwakilishe vyema Taifa la Watanzania kwa kuishangilia Timu yao mpaka Dakika ya Mwisho na kuhakikisha tunapata matokeo Mazuri ya Kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.

    Nae Rais wa Klabu hiyo Engineer Hersi Said ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusikiliza maombi yao na kueleza utaratibu waliouandaa kuelekea Safari hiyo.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.