Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ ) imeahidi kushirikiana na Taasisi ya Farafa Sports Awards kufanikisha Tuzo za wana Michezo Zanzibar zinazotarajiwa kutolewa Mwezi Mei, 2024.
Meneja Masoko na kuendeleza Biashara kutoka Pbz, Seif Suleiman Mohamed huko Mpirani, amesema Benki imeamua kuwaunga Mkono Taasisi ya Farafa ili kufanikisha tukio la utoaji Tuzo za Wanamichezo hapa Zanzibar.
Katibu Mkuu Taasisi ya Farafa Sports Awards, Ali Rashid Pizaro amesema wanaishukuru PBZ na kusema kuwa lengo la tuzo hizo ni kurejesha Hamasa na Mvuto katika Michezo mbali mbali.
Tuzo za Farafa Sports Awards hutolewa kila Mwaka kwa Wanamichezo mbali mbali na Msimu huu wa Tatu zinatarajiwa kufanyika Mwezi Mei.
stories
standard