Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Imejipanga Kuhakikisha Inaweka Mazingira Mazuri Na Wezeshi Kwa Wazee Kwa Kuwajengea Makaazi Mazuri Na Salama Ya Kuishi Ili Kuondokana Na Changamoto Za Makaazi.
Hayo Yameelezwa Na Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Katika Ziara Yake Mkoa Wa Mjini Magharibi Baada Ya Kukagua Mradi Wa Ujenzi Wa Nyumba Za Wazee Welezo.
Amesema Serikali Itaendelea Kuwathamini Na Kuwatunza Wazee Kwa Kuhakikisha Wanapatiwa Mahitaji Yote Muhimu Ikiwemo Kuishi Katika Mazingira Mazuri, Rafiki Na Wezeshi Kulingana Na Uhitaji Wao.
Aidha, Amewataka Wakandarasi Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Huo Ili Uweze Kukamilika Kwa Wakati Na Kwa Kiwango Kilichikusudiwa Ili Kuweza Kutoa Fursa Kwa Wazee Kuhamia Katika Jengo Hilo Na Kisasa Lenye Huduma Zote Za Kijamii.
Kwa Upande Wake Waziri Wa Wizara Ya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Mhe. Anna Atanas Paul Amesema Ni Jambo La Faraja Kuona Serikali Inaendelea Kuwajali Wazee Kwa Kuwajengea Mazingira Mazuri Ya Kuishi Na Huduma Nyengine Za Msingi.
Mhandisi Anna Fransis Kutoka Kampuni Ya Salim Construction Ltd Amesema Jengo Hilo Linalotarajiwa Kukamilika Mwezi Septemba Mwaka Huu Litagharimu Zaidi Ya Shilingi Bilioni 5 Na Litakuwa Na Uwezo Wa Kuchukua Watu Wapatao 112.
Makamu Wa Pili Mbali Na Miradi Aliyoitembelea, Pia Amekagua Ujenzi Wa Chuo Cha Ubaharia Kinachojengwa Bait El Raasi Na Skuli Ya Sekondari Kama Akisema Kuwa Sekta Ya Elimu Ni Nguzo Ya Kutengeneza Wataalamu Nchini.
Miradi Mengine Aliyoikagua Ni Ujenzi Wa Hospitali Ya Ghorofa Ya Kvz—Mtoni, Ujenzi Wa Kituo Cha Afya – Bwefumu, Ujenzi Wa Hoteli Ya Kimataifa Ya Vip- Dimani, Kiwanja Cha Mpira Wa Miguu Kwa Mchina Na Mradi Wa Ujenzi Wa Nyumba Za Bei Nafuu Chumbuni.
