Ibada ya kumuaga aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na WenyeUlemavu) na Mbunge wa Isimani, Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi, inafanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kichangani, Kihesa, Manispaa ya Iringa.
Mwili wa marehemu umeingizwa kanisani kwa heshima kubwa, ukipokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na chama, akiwemo Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, Mwenyekiti wa UWT taifa, Mary Chatanda, Mjumbe wa kamati kuu CCM taifa, Salim Asas pamoja na wanafamilia, ndugu na waombolezaji wengine.
Ibada hiyo imehudhuriwa na mamia ya wananchi waliofika kutoa heshima zao za mwisho, wakikumbuka mchango wake katika uongozi na maendeleo ya taifa.
Mazishi ya Mheshimiwa Lukuvi yanatarajiwa kufanyika kesho kijijini kwao Idodi, mkoani Iringa.
