Waziri Wa Ujenzi Na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed, Amezindua Majaribio Ya Ushushaji Wa Mizigo Katika Bandari Ya Mpigaduri, Zoezi Lililofanywa Na Meli Za Kampuni Ya Azam Marine.
Akizungumza Wakati Wa Uzinduzi Huo Uliofanyika Waziri Wa Ujenzi Na Uchukuzi Ameeleza Kuridhishwa Na Majaribio Hayo, Huku Akisema Ni Sehemu Ya Jitihada Za Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Kupunguza Msongamano Katika Bandari Ya Malindi.
Amesema Kazi Rasmi La Ushushaji Mizigo Inatarajiwa Kuanza Mwezi Aprili Mwaka Huu Baada Ya Kukamilika Kwa Majaribio Ya Awali.
Kwa Upande Wake, Meneja Wa Azam Marine, Ali Mohamed, Amesema Bandari Hiyo Itasaidia Kupunguza Muda Wa Kushughulikia Mizigo Na Kuongeza Ufanisi Wa Kazi.
Mkurugenzi Mkuu Wa Shirika La Bandari Zanzibar, Akif Ali Khamis, Amesema Bandari Hiyo Imejengwa Na Kampuni Ya Zf Devco Kwa Kushirikiana Na Serikali, Ikiwa Ni Sehemu Ya Kuboresha Miundombinu Ya Usafiri Visiwani Zanzibar.
Ujenzi Wa Bandari Ya Mpigaduri Unatajwa Kuwa Hatua Muhimu Katika Kukuza Uchumi Na Kuboresha Huduma Za Usafiri Wa Baharini Zanzibar.
