ZBC IMETIA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI COMORO

ZBC NA COMORO

    Katika kuendeleza Ushirikiano wa Zaidi ya Miaka 15 kati ya Tanzania na Comoro, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limetia Saini Mkataba wa Ushirikiano na Shirika la Utangazaji Comoro ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu. 

    Kwa upande wa ZBC Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Ndg.Ramadhani Bukini na kwa upande wa Comoro amesaini Balozi wa Comoro Nchini Tanzani Dkt.Ahmada Mohammed.

    Akizungumza baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo Mkurugenzi Bukini amesema Mkataba huo wa Mashirikiano ya Miaka Mitano utakwenda kukuza Viwango, Mbinu na Ubunifu kwa Waandishi wa Habari kutoka pande zote Mbili.

    Zoezi hilo la Utiaji Saini Limeshuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Comoro Mhe. Mbae Mohamed walipata nafasi ya kuzungumza machache  kuhusu mkataba huo

    Jumla ya Mikataba Minne imetiwa Saini za Makubaliano katika Sekta ya Ushirikiano wa Kidipolamasia, Afya, Biashara, Viwanda na Teknolojia ya Habari, ndani ya kilele cha Mkutano wa Kwanza wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano (JPC) Uliofanyika Jijini Dar es salaam

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.