Wizara ya Maji, Nishati na Madini imetiliana Saini Hati ya Makubaliano na Kampuni Mbili kutoka Nchini China kwa ajili ya Mkataba wa Kazi ya Ujenzi wa Miundo mbinu ya Umeme.
Akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini huo Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema Mradi huo wa kupitisha laini za Umeme na kupoozea Umeme huko Makunduchi na Matemwe utaisaidia Zanzibar kuondokana na tatizo la Umeme mdogo pamoja na upotevu wa Umeme unaojitokeza katika Maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi Wizara ya Maji Nishati na Madini Said Mdungi na Meneja Mkuu Shirika la Umeme Zanzibar Ndg. Haji Haji wamesema kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kuleta Mapinduzi katika Sekta ya Umeme, kuvutia Uwekezaji wa Viwanda vya kati pamoja na kuzalisha ajira kwa Vijana.
Nao Wawakilishi wa Kampuni ya JV, ZTT na Sieyuan kutoka China wamesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika nyanja mbali mbali ili kuleta Maendeleo kwa Wananchi wake.