Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Tanzania sekta ya Sukari ni kipaumbele katika ukuzaji wa maendeleo ya Viwanda Nchini .
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Mkutano wa Wazalishaji Sukari wa Nchi za SADC katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliopo Uwanja wa ndege Zanzibar.
Amesema Tanzania imeweka Mazingira wezeshi ya uwekezaji katika Kilimo cha Miwa na uzalishaji Sukari na kutoa Rai kwa Nchi za SADC kutumia fursa zilizopo kwa kuweka Mazingira bora zaidi ya uwekezaji ili kukuza uzalishaji wa Sukari.
Dkt.Mwinyi amewataka Washiriki wa Mkutano huo kuwekeza katika Teknolojia za kisasa na mbinu za Kilimo za kisasa zinazoongeza tija ili kuimarisha mavuno ya Miwa na uzalishaji Sukari Afrika.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Suleiman Jafo amesema Viwanda vya uzalishaji Sukari ni miongoni mwa mpango mkakati wa Serikali wa maendeleo ya Viwanda Nchini kuanzia 2015/63.
Waziri wa BIashara na maendeleo ya Viwanda wa SMZ, Mh. Omar Said Shaaban amewataka wawekezaji kuitumia fursa iliopo kwa kuekeza Zanzibar.
Seif Ali Seif, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari Tanzania ameziomba Serikali zote mbili kupitia Taasisi zenye Mamlaka ya kuandaa Sera Sheria na kanuni kuweka Sheria zisizo nyepesi zitakazowavutia wawekezaji zaidi.