Akizundua Ndege ya Jambojet Q400 ambayo itaanza safari zake kutoka Mombasa Kenya kuja Zanzibar katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi DkT.Khalid Salum Muhammed amesema hatua hiyo itachangia kukuza Uchumi hasa kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wanatoa bidhaa zao Mombasa Kenya kwa kutegemea Majahazi.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga amesema kuwepo kwa Ndege hiyo kutachangia kuifunguwa Zanzibar katika Sekta ya Utalii katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Jambojet Karanja Ndegwa amesema lengo la Kampuni yao ni kuunganisha Afrika Mashariki katika Sekta ya Usafiri wa Anga ili Abiria wanaotumia Sekta hiyo wapate Huduma iliyo bora .
Ndege ja Jambojet imeanza Huduma zake rasmi Zanzibar ambapo Abiria zaidi ya 80 wataweza kusafiri katika kila Siku ya Jumatatu Jumatano Ijumaa na Jumapili.