Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Imechukua Hatua Thabiti Ya Kuweka Mazingira Bora Ya Kufanyia Kazi Kwa Mhimili Wa Mahakama.
Amesema Katika Mwaka Wa Fedha 2025/2026 Serikali Imewekeza Zaidi Ya Fedha Za Kitanzania Shilingi Bilioni 13.6 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Majengo Ya Kisasa Ya Mahakama Ambayo Yanaendana Na Uwekaji Wa Miundombinu Ya Tehama.
Baada Ya Shamrashamra Ya Wiki Ya Sheria, Hatimae Kilele Cha Maadhimisho Hayo Yamefanyika Kisiwani Pemba.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Ameongoza Maadhimisho Hayo Kwa Niaba Ya Rais Wa Zanzibar, Amesema Azma Ya Kuleta Ufanisi Wa Majukumu Katika Mahakama Itachangiwa Na Matumizi Ya Tehama Ili Kurahisisha Huduma.
Hata Hivyo, Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Ameupongeza Uongozi Wa Mahakama Kuu Ya Zanzibar Kwa Kuifanyia Kazi Sheria Ya Mwenendo Wa Madai Ya Zanzibar (Civil Procedure Decree Chapter 8) Ya Mwaka 1917 Ambapo Rasimu Ya Sheria Mpya Na Kanuni Kadhaa Zimeshatayarishwa.
Jaji Mkuu Wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla Amesema Mifumo Mitano Imeundwa Kwa Ajili Ya Kurahisisha Utendaji Kazi Wa Mahkama Ikiwemo Mfumo Wa Usimamizi Wa Mashauri Ambao Utazifanya Mahkama Kuondokana Na Matumizi Ya Makaratasi Na Mawakili Watafungua Mashauri Ya Kesi Bila Ya Kufika Mahakamani.
Nae Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi Na Utawala Bora Dkt. Haroun Ali Suleiman Amesema Wizara Hiyo Itaendelea Kushirikiana Na Watendaji Wa Mahkama Kuhakikisha Wanafanya Kazi Katika Mazingira Bora.
