DK MWINYI AMEPONGEZA UHUSIANO ULIOPO BAINA YA TANZANIA NA UAE.

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi amepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hasa Zanzibar na umoja wa Nchi ya Falme za Kiarabu - UAE.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipokutana na Mhe Ali Rashid Alnuaimi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya UAE.

Rais Dk Hussein Ali Mwinyi ameelezea kufurahishwa na wawekezaji wanaoounga mkono miradi mbalimbali ya Zanzibar, wakiwemo Wafanyabiashara kutokea umoja huo wa Falme za kiarabu.

Mbali na hayo Dk. Mwinyi amemueleza Mgeni wake kuwashajihisha wawekezaji zaidi kuja kuwekeza Zanzibar. 

Kwa upande wake Mhe Alnuaimi amesema wakati umefika kwa Viongozi kufanya kazi kwa bidii na kasi kubwa kwa manufaa ya Nchi zao ili Wananchi wao wanufaike na Rasilimali zao.

Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu U.A.E unajumuisha Abudhabi, Dubai, Sharjah, Ras al Khaimah, Ajman, Fujairah na Ummul Quweiyn.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.