Akizungumza katika Mkutano wa 41 wa Taasisi ya usimamizi wa kumbukumbu Afrika RMFA Muandaaji wa Mkutano huo unaofanyika Zanzibar kwa mara ya Tatu Grace Donath Kaganga amesema utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kupitia Mfumo wa Kieletroniki unahakikisha usalama zaidi dhidi ya madhara mbalimbali.
Washiriki wa Mkutano huo wamesema Mafunzo wanayoyapata yatawasaidia kuongeza taaluma juu ya Utunzaji wa Kumbukumbu Kielektorini na kuahidi kutekeleza kwa vitendo ujuzi huo Wakirejea Nchini kwao.
Taasisi ya RMFA ina uzoefu wa Takriban Miaka 20 katika kutengeneza bidhaa za kipekee za Kidigitali na Majukwaa ambapo inajihusisha na usimamizi wa Maktaba, Mafunzo ya Kieletroniki, Mikutano ya Kimataifa Usimamizi wa Kumbukumbu na muundo ya mifumo.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni " Mifumo Jumuishi ya Usimamizi wa Kumbukumbu za Kieletroniki "