UTUNZAJI KUMBUKUMBU WA KIELETRONIKI UTASAIDIA KUENDANA NA MABADILIKO YA UCHUMI WA KIDIGITALI AFRIKA

RMFA

   Taasisi za Umma na Binafsi zinashauriwa kutumia Mfumo wa  Kieletroniki katika utunzaji wa kumbukumbu ili kuendana na mabadiliko ya uchumi wa kidigitali Barani Afrika.

    Akizungumza katika Mkutano wa 41 wa Taasisi ya usimamizi wa kumbukumbu Afrika RMFA Muandaaji wa Mkutano huo unaofanyika Zanzibar kwa mara ya Tatu Grace Donath Kaganga amesema utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kupitia Mfumo wa Kieletroniki unahakikisha usalama zaidi dhidi ya madhara mbalimbali. 

    Washiriki wa Mkutano huo wamesema Mafunzo wanayoyapata yatawasaidia kuongeza taaluma juu ya Utunzaji wa Kumbukumbu Kielektorini na kuahidi  kutekeleza kwa vitendo ujuzi huo Wakirejea Nchini kwao.

   Taasisi ya RMFA ina uzoefu wa Takriban Miaka 20 katika kutengeneza bidhaa za kipekee za Kidigitali na Majukwaa ambapo inajihusisha na usimamizi wa Maktaba, Mafunzo ya Kieletroniki, Mikutano ya Kimataifa Usimamizi wa Kumbukumbu na muundo ya mifumo.

   Kauli mbiu ya Mkutano huo ni " Mifumo Jumuishi ya Usimamizi wa Kumbukumbu za Kieletroniki "

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.