Jumuiya inayojishughulisha na huduma za Jamii Directaid Zanzibar imechinja Ng’ombe 35 kwa ajili ya kutoa sadaka ya Sikukuu ya Eid El -Adhaha ikiwa ni utaratibu wa kila ifikapo mfunguo Tatu.
Akizungumza na ZBC katika machinjio ya kisakasaka Afisa wa Manunuzi wa Jumuiya hiyo ali Suleiman Ali amesema Jumuiya hiyo itaendelea kutoa Sadaka hiyo maeneo ya Mjini pamoja na Vijijini ili Jamii iweze kukidhi mahitaji ya SIkukuu.
Daktari wa Mifugo kutoka Wakala wa Chakula na Dawa Thamra Khamis Talib amewatoa hofu Watumiaji wa nyama ya Ng’ombe ambao Wanachinjwa eneo hilo la Kisakasaka na kusema kuwa wamezingatia ubora baada ya kufanyiwa Uchunguzi
Mwenyekiti wa Wachinjaji Idrisa Othman Iddi amesema kazi ya Uchinjaji imekwenda vizuri pamoja na kukabiliwa na Tatizo la Miundombinu pamoja na uchakavu wa Jengo Wanalofanyia kazi hiyo.
Wananchi wanaofuata kupata Sadaka ya Nyama wameomba kuwekwa kwa utaratibu maalum utakaosadia kupuinguza usumbufu wa kusubiri kwa muda mrefu.