UJENZI WA BARABARA TUNGUU-MAKUNDUCHI WAIVA

MECCO
English

Asilimia 45 ya Vifaa vitakavyotumika kataika Ujenzi wa Barabara ya Tunguu- Makunduchi na Fumba Kisauni vimekamilika tayari kuanza Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Muhamed amekagua Kambi ya Mecco, Kampuni inayojenga Barabara hizo nakueleza kuridhishwa kwake na matayarisho yalifofanyika.

Hii si Biashara ya Gari lakini ni Kambi maalum ya Ujenzi wa Barabara ya Urefu wa Kilomita 48 ya Tunguu-Makunduchi na Barabara ya Fumba Kisauni yenye Urefu wa Kilomita 12.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Badria Atai Masoud, anasema moja ya faidaya uwepo wa Ujenzi huu ni kutengeneza Ajira kwa Vijana wazawa.

Kampuni ya Mecco inayofanya Ujenzi huo imesema, Ujenzi wa Barabara zote Mbili utaenda kwa pamoja kwa mgawanyo maalum. “ Tumegawanya Ujenzi huu katika Sehemu Mbili ya Tunguu na Fumba, Sehemu ya kwanza ya Ujenzi itakuwa ya umbali umbali wa Kilomita 14 na tutafanya hivyo baada ya kufata utaratibu wa Makazi katika Eneo hilo”.

“ Ujenzi wa Barabara ya Fumba Kisauni, Ujenzi wake utahusisha Urefu wa Kilomita Tano za Awali.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.