ZMOTION NA TIGO PESA KUANZISHA MFUMO WA LIPA ADA NA SKULI BINAFSI

WAZIRI LELA

    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Lela Mohammed Mussa amewaomba Wamiliki wa Skuli Binafsi kukaa pamoja na Wazazi kwa ajili   ya ulipaji Ada ya Masomo pindi Mwanafunzi anapochelewa kulipiwa Ada hiyo.

    Akizindua huduma ya Lipa Ada kwa Skuli Binafsi Waziri Lela amesema huo ni ubunifu wa Teknolojia  ambao utarahisisha  kutumika utendaji  katika Sekta ya Elimu.

   Amesema suala la kulipa Ada ni la Mzazi na sio Mwanafunzi hivyo si vyema kuwanyanyasa Wanafunzi ikiwemo kuwatoa Madarasani wanapochelewa kulipiwa Ada hiyo.

    Afisa Mkuu Tigo Pesa  Angelica Pesha amesema Mfumo huo utaondoa usumbufu kwa Wazazi na Walimu kupata suluhisho kwao na kuleta  ufanisi katika Elimu.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Zmotion Taasisi inayojishughulisha na Mifumo (Zmotion) Ndg.Said Hemed Ali amesema  wameamua kuleta mfumo huo ili kuisaidia Serikali katika kufanya kazi Kidigitali

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.