WAHITIMU WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUTAFUTA FURSA ZA MASOMO

Feza School

    Kamishna wa Polisi Zanzibar CP.HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka wanafunzi wanaomaliza masomo nchini wasijiingize kwenye makundi ya kihalifu na badala yake watumie fursa za kimasomo zinazotolewa na nchi mbalimbali kupitia mtandao ili kujiendeleza Zaidi na Masomo.

    Akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi katika Mahafali ya Mwaka 2024 ya Skuli ya Feza Zanzibar amesema ni vyema kwa vijana hao kuwa na maadili mema, waaminifu na waadilifu kwani Taifa lina matarajio makubwa kutoka kwao.

    Akisoma risala ya Wazazi wa Skuli hiyo MGENI ASAA amewataka wazazi na walezi kuwasimamia watoto na kuwapa mwongozo ili kufikia malengo yao.

    Katka Risala ya Wanafunzi wanaohitimu iliyosomwa na Mwanafunzi MARIYAM HAMAD KHAMIS wamewashukuru wazazi na walimu katika kuwasimamia na kuwatia moyo na hatimae kukamilisha masomo yao ya Kidatu cha sita kwa Mafanikio.

Jumla ya wanafunzi 42 wamehitimu Kidatu cha sita Skuli ya FEZA Zanzibar mwaka 2024.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.