Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Wadau wa Sekta ya Anga kuimarisha Mashirikiano ili kuhakikisha Sekta hiyo inazidi kuimarika.
Akifungua Kongamano la Sita la Usafiri wa Anga la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Verde Mtoni,Dk.mwinyi, amesema Nchi inajivunia mafanikio yaliofikiwa katika sekta hiyo.
Amesema usafiri wa Anga ndio kichocheo kikubwa cha ukuaji wa Uchumi, hivyo ni vyema kukawepo Mashirikiano yapamoja kwa maslahi ya Taifa.
Aidha Dk.Mwinyi, amesema katika kufikia malengo yaliowekwa katika ukuaji wa Sekta ya Utalii ni muhimu kuisaidia Sekta ya usafiri wa Anga kuzidi kuimarika.
Amefahamisha kuwa Malengo ya Cossoa ni kusaidia Nchi Wanachama katika kutimiza Majukumu ya udhibiti wa usalama chini ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mkataba wa chicago.
Hivyo amesema Nchi inaendelea kunufaika na uhusiano Mzuri wa Nchi zote Wanachama kwa kuzingatia Dira ya pamoja kwa madhumuni ya usalama wa Anga kwa maendeleo ya Mataifa.
Mapema Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dr.Khalid Salum Mohammed, amesema Watu wengi wanafikiria usafiri wa Anga ni salama na haraka, hivyo ni muhimu Wadau wakawa na
uwelewa wa kutosha juu ya mada ya Usalama ambayo itazungumziwa katika Kongamano hilo.
Kwa Upande wake Spika wa Bunge la Afrika mashariki,mh. Joseph Ntakiruimana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari,wamesema tayari wameanzisha jumuiya ya Anga ili kusaidia kukuza Uchumi na kuwa endelevu