Taasisi ya Tulia Ttrust imetoa msaada wa kumjengea Nyumba ya kuishi Mama Mjane Singwava Jackson kwa lengo la kumpunguzia shida na Familia yake.
Akikabidhi Nyumba hiyo Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust Dkt. Tulia Ackson amesema Taasisi yake itaendelea kusaidia Jamii hasa Watu wenye mazingira magumu
Dkt. Tulia ambae ni Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Tanzania amemkabidhi Fedha Taslim kuanza mtaji wa kuendeleza maisha yeye na Familia yake ya Watoto Sita Amesema mpango huo utasaidia kuwaondolea shida Wananchi wake pamoja na kuwarahisishia mazingira ya Maisha yao.
Akitoa Shukrani zake Singwava Jackson Mjane mwenye Watoto Sita Mkaazi wa Kata ya Iganjo Jijini Mbeya amesema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akipambana na kuwaendeleza Watoto wake katika mazingira magumu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amempongeza Dkt. Tulia kwa kugusa Maisha ya Watu wenye uhitaji.
Baadhi ya Majirani waliohudhuria hafla hiyo wamesema kuwa Mama huyo anastahili kusaidiwa kutokana na mazingira magumu anayoishi..
Awali kabla ya kukabidhiwa Nyumba Bi Singwava Jackson alikuwa anajishughilisha na kulea Familia kwa kazi ya kuokota Makopo na anaishi kwenye Nyumba aliyojenga kwa Maturubai kwa Takribani Miaka Miwili.