TARURA YABAINI MADARAJA 19 YAMESOMBWA NA MVUA RUVUMA

Wahandisi kutoka TARURA Daraja la Njoke

     Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoani Ruvuma imebaini Jumla ya Madaraja 19 ambayo yamesombwa na Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani hapo katika Ripoti iliyosomwa kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo mtela Mwampamba.

    Kwa upande wake Mhandisi  Silvanus Ngonyani Kaimu  wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanazania (TARURA) amewahakikishia Wananchi kwamba TARURA ipo kazini hivyo sio tu wameishia Daraja la Mto Njoka bali wanaendelea kurekebisha mitandao yote ya Barabara ambazo ni korofi huku akihusisha na Daraja ambalo linafanyiwa usanifu ili waanze kulirekebisha

     Hata hivyo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndg.Mtela Mwampamba amesema licha ya Mkoa kuwa katika nafasi nzuri ya uzalishaji wa mahindi hivyo amewataka Wananchi kutozichukia Mvua kwani mvua ni baraka hivyo waendelee na uzalishaji wa mazao yao bali kuhusu suala la Madaraja Serikali sikivu ya awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan itahakikisha inayatengeneza

     Naye Ndg. Noel Nombo ameipongeza TARURA  kwa ujenzi wa Daraja hilo ambalo hapo hawali walipata changamoto ya Watoto kuto kwenda Shule kwa wakati klutokana na ukosefu wa Madaraja

    Vilevile Ndg.Monica Hinju yeye amempongeza na kumshukuru kwa dhati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kwakusimamia vyema utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa Daraja hilo la Njoka

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.