Hatua kali za Kisheria zitawachukulia kwa Wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na Bei elekezi ya Sukari iliyowekwa na Serikali .
Tume ya Ushindani Halali wa Biashara imelifunnga Duka la Mfanyabiashara wa bidhaa ya Sukari huko Saateni kwa kuuza bidhaa hiyo Kinyume na Bei elekezi.
Akichukua hatua hiyo Mkurugenzi wa kumlinda Mtumiaji na udhibiti wa Bidhaa Bandia Tume ya Ushindani halali wa Biashara Ndg. Aliyah Emmanual Juma amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini Mfanyabiashara Sultan Seif Muhammed kuuza Sukari kinyume na sheria.
Mfanyabiashara wa Duka hilo la Sukari Sultani Seif Muhammed amedai kuwa hawahusiki na shutuma za Tume kutokana na kuwa na vielezo vya kisheria katika Biashara yao.
Awali katika hali iliyomshitua mnunuzi Ndg.Issa Hassan Issa katika Duka hilo amedai kununua Sukari kwa Bei ya juu