MFANYABIASHARA WA SAATENI ASHUTUMIWA KUUZA SUKARI KINYUME NA BEI ELEKEZI

TUME YA USHINDANI WA BIASHARA

    Hatua kali za Kisheria zitawachukulia kwa Wafanyabiashara wanaokwenda kinyume na Bei elekezi ya Sukari iliyowekwa na Serikali .

    Tume ya Ushindani Halali wa Biashara imelifunnga Duka la  Mfanyabiashara wa bidhaa ya Sukari huko Saateni kwa  kuuza bidhaa hiyo Kinyume na Bei elekezi.

    Akichukua hatua hiyo Mkurugenzi wa kumlinda Mtumiaji na udhibiti wa Bidhaa Bandia Tume ya Ushindani halali wa Biashara   Ndg. Aliyah Emmanual Juma amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini Mfanyabiashara Sultan Seif Muhammed kuuza Sukari kinyume na sheria.

    Mfanyabiashara  wa Duka hilo la Sukari Sultani Seif Muhammed amedai kuwa hawahusiki na shutuma za Tume  kutokana na kuwa na vielezo vya kisheria katika Biashara yao.

    Awali  katika hali iliyomshitua  mnunuzi Ndg.Issa Hassan Issa  katika Duka hilo amedai kununua  Sukari kwa Bei ya juu 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.