MRADI WA KUFUNGA KIFAA MAALUMU KATIKA MELI ZA UVUVI WASAINIWA

UTIAJI SAINI MRADI WA VIFAA KATIKA MELI ZA UVUVI

     Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu wamesaini hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka hiyo na Mradi wa Usaid Heshimu Bahari  Chemonic International INC ili kuimarisha usimamizi wa Rasilmali za Bahari kwa kufunga kifaa maalumu kitakachoonyesha uhalisia wa sehemu utakayovua.

    Wakisaini  Hati ya Ushirikiano  huo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ndg. Emanuel Andrew Sweke amesema Kifaa hicho  kitasaidia  Sekta ya Uvuvi kupunguza kuvua Uvuvi haramu na kuzuwia mianya ya upotevu wa rasilmali za bahari zisipotee.

     Msimamizi wa Mradi wa Usaid Heshimu Bahari Mathias lgulu amesema Mradi wa Usaid Heshimu Bahari utaleta manufaa kwa Serikali zote mbili katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Nchi kupitia Uvuvi wa Bahari kuu.

     John Koma kutoka  Usaid Heshimu Bahari amesema Mradi huo wa ufungaji kifaa katika Meli za Uvuvi utaonesha Matukio yote ya Baharini yanayofanywa na Meli za Kigeni na za ndani ya Nchi.

      Mradi huo wa mipaka Mitano utagharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 25  ambapo zaidi ya Meli 48 zimepatiwa Leseni  zikiwemo za Tanzania.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.