Wakisaini Hati ya Ushirikiano huo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ndg. Emanuel Andrew Sweke amesema Kifaa hicho kitasaidia Sekta ya Uvuvi kupunguza kuvua Uvuvi haramu na kuzuwia mianya ya upotevu wa rasilmali za bahari zisipotee.
Msimamizi wa Mradi wa Usaid Heshimu Bahari Mathias lgulu amesema Mradi wa Usaid Heshimu Bahari utaleta manufaa kwa Serikali zote mbili katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Nchi kupitia Uvuvi wa Bahari kuu.
John Koma kutoka Usaid Heshimu Bahari amesema Mradi huo wa ufungaji kifaa katika Meli za Uvuvi utaonesha Matukio yote ya Baharini yanayofanywa na Meli za Kigeni na za ndani ya Nchi.
Mradi huo wa mipaka Mitano utagharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 25 ambapo zaidi ya Meli 48 zimepatiwa Leseni zikiwemo za Tanzania.