Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani umetoa Vifaa kwa Mama na Watoto waliozaliwa.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa Niaba ya ZSFF Ndg.Zainab Rajab Baraka amesema lengo la kufanya hivyo ni kuthamini mchango wa Wanawake katika Jamii hasa katika vikwazo vinavyowakumba na kuweza kukabiliana navyo
Wauguzi Wakuu Hospitali ya Kivunge na Magogoni Ndg. Kulthum Ramadhan Said na Ndg.Mwanavua Said Nassor wamesema kina Mmama baada ya kujifungua wanahitaji zaidi vifaa vya usafi hivyo kuwapatia Zawadi hizo kutasaidia kuimarisha usafi wa Mama na Mtoto
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Wazazi Ndg.Patima Nipewa Haji amewapongeza Watendaji hao kwa kuwathamini na kuwajali.
Hospitali zilizotembelewa ni Kivunge na Magogoni ambapo Waliojifungua walipatiwa Sabuni Nguo na Pempas