Zaidi ya Wanafunzi 1500, wa Shule ya Msingi Ludeba katika Kijiji cha Ludeba, Kata ya Ipalamasa, Wilaya ya Chato Geita wanakabiliwa na ukosefu wa Vyoo vya kisasa hali inayosababisha taaluma kushuka.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Deusdedith Katwale amewashauri Wananchi wa Kata ya Ipalamasa kuhakikisha anasimamia upatikanaji wa huduma muhimu katika Shule ya Msingi Ludeba na Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbinu ya huduma za Kijamii.
Deusdedith amebainisha hayo wakati wa Ziara ya kutembelea Shule za Kata ya Ipalamasa kuona maendeleo ya Kijamii katika Wilaya hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hio Ndg.Daudi William amesema kuwa Shule yake inakabiliwa na tatizo la Vyoo na kusababisha mahudhurio ya Wanafunzi kuwa mabaya..
Afisa Elimu Wilaya ya Chato Ndg.Theobad Katama amewaomba Wananchi kushirikiano na kufanya utaratibu wa kusaidia kutatua tatizo hilo.