DKT. MWINYI ATOA POLE KWA MSIBA WA EDWARD LOWASSA

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameungana na Viongozi wa Chama, Serikali na wakaazi wa Jiji la Dar Es Salaam kutoa Mkono wa pole katika Msiba wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowasa.

Akiwa ameambatana na Mkewe Mama Maryam Mwinyi Raisi Mwinyi amemuelezea Hayati Edward Lowasa kuwa ni Kiongozi

Mbali na Raisi Mwinyi Viongozi wengine waliofika kutoa Mkono wa pole na kusaini Kitabu cha maombolezo ni Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdullah, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na uratibu Mh.Jenista Mhagama, Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, na Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Paul Makonda.  

Mwili wa Marehemu Edward Lowasa unatarajiwa kuzikwa February 17 Wilayani Monduli Mkoa wa Arusha ambapo kesho Mwili huo unatarajiwa kuwagwa katika Viwanja vya karijee Kijini Dar Es Salaam.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.