MKURUGENZI TCRA ATHIBITISHA UWEPO WA TATIZO LA KIMTANDAO NCHINI

Dkt.Jabir Bakari

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari amesema tatizo la Mtandao kukwama siku ya leo imetokana na Miundombinu ya Intaneti na sio kifaa unachokutumia (Simu).

     " Kunaonekana kuna tatizo la kiufundi kidogo linalohusiana na 'marine cables' kwa hiyo tunajaribu kupata maelezo zaidi," amesema Dk Bakari.

    Dk Bakari amesema kwa sasa wanatazama namna ya kupata taarifa zaidi ili kujua ilipo changamoto ili kuchukua hatua.

    Tatizo la mtandao wa intaneti limeanza tangu saa 4 asubuhi na kutengeneza taharuki kwa watumiaji wa mitandao ya simu mbalimbali nchini.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.