Kampuni ya Sarnity Tour wamekabidhi Vifaa vya Michezo kwa Waraibu wa Kitengo cha Tiba, Kinga na Kurekebusha Tabia Kidimni ili kutoa fursa ya Michezo Kituoni hapo.
Wakikabidhi Vifaa vya Michezo katika Kituo cha kinga Tiba na kurekebisha tabia Meneja wa Kampuni ya Sarnity Ndg. Florence Agustino amesema lengo la kutoa Vifaa hivyo ni kutoa Fursa kwa Waraibu wa Kituo hicho ili kushiriki Michezo wakat wakiendelea na kupatiwa Elimu juu ya kuchana na utumiaji wa Madawa ya kulevya.
Kamishna wa Kinga tiba na kurekilebisha tabia Ndg.Juma Zidi Kheir Ameushukur Uongozi wa Kampuni hiyo na kuzikarbisha Taasisi nyengine na kutoa wito kwa Wahanga wa Matumizi ya Madawa ya kulevya kujiunga ili kuikomboa Jamii katika vitendo viovu
Nae Nahodha wa Timu ya Kitengo hicho amesema vifaa hivyo vitasaidia kuinua Timu yao na kukuza Michezo Kituoni hapo
vifaa vilivyokabidhiwa ni Mipira na Jezi