Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ni muhimu kuimarisha Mifumo ya Afya katika Ngazi zote hususani huduma za Afya ya Msingi ili kudhibiti hatari za Kiafya katika Jamii.
Makamu wa rais amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Afya Kanda ya Afrika Mashariki, kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha.
amesema katika Ukanda unaohudumiwa na taasisi hiyo, ipo haja zaidi ya kuimarisha utayari wa kukabiliana na dharura za Kiafya, uhimilivu na urejeshaji hali ya kawaida baada ya tatizo ili kupunguza athari za dharura katika ukanda huo.
Nae Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amezishukuru Serikali za Nchi Wanachama kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya Afya Licha ya uwepo wa vipaumbele vingi katika mataifa hayo. Amesema kwa Miaka mingi mapendekezo mbalimbali yamepitishwa kwa lengo la kuimarisha sekta ya Afya na ustawi wa Watu.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mawaziri wa Afya, Wadau wa Sekta ya Afya na Wataalam mbalimbali kutoka Mataifa ya Afrika.