Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar kupitia Kamati ya Soka la Ufukweni imeandaa Mashindano ya Kimataifa ya Mpira wa Ufukweni kwa lengo la kuvitangaza vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini.
Akitoa taarifa mbele ya Vyombo vya Habari, katibu Kamati ya Soka la ufukweni Zanzibar, Ali Sharifu Adolf, huko Mbuyu Mnene.
Amesema Mashindano hayo yatashirikisha timu 4 kutoka Unguja na yatafanyika katika Fungu la Mchanga la Nakupenda Sand Bank.
Adolf amewaomba Wahisani na Wadhamini mbali mbali kuwaunga mkono ili kufikia lengo la Mashindano hayo.
Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni, Abdullatif Mwinyi amesema Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na Mvuto wa pekee kwa wenyeji na Wageni.
Timu zitakazoshiriki Mashindano hayo ni Malindi Beach Soccer Club, Suluhu Academy, Kaskazini Unguja na Kisauni Beach Soccer.