MANISPAA YA LINDI YAINGIA MAKUBALIANO YA BIASHARA YA HEWA UKAA

Viongozi Manispaa Lindi

      Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Lindi  limepitisha mkataba wa makubaliano ya Biashara ya hewa ukaa katika vijiji 10 , jumuhiya za uhifadhi wa Misitu 3  na msitu wa hifadhi wa manispaa na kampuni ya village climate solution limited (VCSL).

       Wakizungumza katika kikao cha robo ya tatu ya baraza hilo ,  madiwani  hao wamesema kuwepo kwa biashara hiyo kutaiongezea Halmashauri chanzo kipya cha mapato na kwamba mradi huo utakuwa na manufaa kwa Manispaa na wananchi kwa ujumla

     Meneja wa Mradi huo  yahya Mtonda amesema Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi kisichopungua miaka 40 katika Vijiji   vya Kiwawa, Mputwa, Milolo magharibi, Ruhoma, Muungano, Kinyope, Likwaya, na Makumba.

      " sambamba na vijiji hivi mkatamba huu umeusisha jumuhiya za uhifadhi wa Misitu ambazo zimeanzishwa pembezoni mwa Mtaa wa Nandambi, pamoja na msitu wa hifadhi wa Makangara katika Manispaa hii ya Lindi nao pia umeingia katika Biashara ya hewa ukaa"

     Amesema  miongoni mwa sababu ya mradi huo kutekelezwa kwa miaka 40  ni kufanya ulizi wa Misitu hiyo kwa muda mrefu  ili kupunguza hewa ukaa kwa kuhifadi  Misitu hiyo ili viweze kuwasaidi vizazi vya sasa na vijavyo.

      " ki asili misitu inaweza kuishi kwa muda mrefu hivyo basi kutokana na sababu hiyo basi miti inaweza kuendelea kuruhusu kufanyika kwa biashara hii ya hewa ukaa kwa kipindi hiko cha miaka 40

    Kama tutaweza kuwezesha malipo ya fedha zinazotokana na biashara ya hewa ukaa kwa  kipindi cha miaka 40 basi fedha zile zitaenda kwenye shughuli mbalimbali za vile vijiji na ni matumaini yetu vijiji vitaenda kukua kwa kuboresha vijiji vyao

   Pamoja na kusaidi makubaliano hayo pia Baraza limepitisha  mipango na sheria ndogo za uhifadhi wa Misitu kwa kijiji cha Milola, Mputwa na kijiji cha Namtamba  baada ya kusaidiwa na shirika la kuhifadhi misitu tanzania TFCG kuanzisha misitu ya hifadhi kwa kufanya matumizi bora ya Aridhi ya vijiji vyao kwa kipindi cha miaka 40.

 

 

 

 

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.