MAMA MARIAM MWINYI ATOA SHUKURANI KWA SERIKALI YA KOREA

Mama Mariam Mwinyi

     Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)  Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameishukuru  wadau wa maendeleo wa Korea kupitia Jumuiya ya Lady Fatima Charity kwa msaada  wa dola za kimarekani 37,000  kwa ajili kuwezesha upatikanaji wa  kutoa Taula za kike (Tumaini Kits)  zinazotengenezwa na ZMBF na zimenufaisha zaidi ya Wasichana 2500 wa shule za Pemba.

     Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipokutana na  Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya kudumu ya Bunge la Korea , Mhe.Sul Hoon na ujumbe wake waliofika ofisini kwake Ikulu Migombani tarehe: 11 Mei 2024.

     Mama  Mariam Mwinyi amesema ndoto yake ni kuwasaidia kuwainua kiuchumi Wanawake  hususani wakulima wa Mwani kwa kuanzisha kiwanda kidogo cha kuchakata zao hilo , na amewakaribisha Serikali ya Korea  katika kuendeleza ushirikiano na kujifunza zaidi kutoka kwao.

     Naye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya kudumu ya Bunge la Korea , Mhe.Sul Hoon  na ujumbe wake wameahidi kushirikiana na Taasisi ya ZMBF katika nyanja mbalimbali hususani vipaumbele vya Taasisi hiyo .

      Wabunge wengine walioshiriki ni pamoja na  Mhe. Lee Hunseng na Mhe.Shin Hyun Young kutoka Bunge la Korea wanaojishughulisha na masuala ya mashirikiano na Bara la Afrika pia Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe.Kin Sun Pyo ameambatana na ugeni huo.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.