MACHICHA YAIGARAGIZA B5 MASHINDANO YA SWALA AIR CARCO

Michezo

     Timu ya Mpira wa Miguu ya Machicha FC  imefanikiwa kuondoka na ushindi wa Penalty 5-4 dhidi ya Timu ya B5, katika Michuano ya Swala Air Cargo Ndg.Ramadhan CUP, yanayoendelea Viwanja vya Mau.

    Mchezo huo uliokuwa mgumu kwa Timu zote Mbili Mbili, licha ya Mashambulizi ya mara kwa mara, lakini kila mmoja alilinda vyema lango lango lake lisitikiswe wavu, na kupelekea Dakika 90 kukamilika kwa Sare Tasa ya bila ya kufungana.

    Hatua ya changamoto ya Mikiwaju ya Penalty ikachukua Nafasi, na Timu ya Machicha kufanikiwa kuondoka na ushindi wa Penalty 5-4 Uwanjani hapo.

      Nahodha wa Timu ya Machicha, Ahmed Bolo na Nahodha wa B5 Daudi maridadi wamesema Mchezo ulikua mzuri na kiula mmoja ametumia nafasi alizotengeneza.

    Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Swala Air Cargo ambao ndio, Waanzilishi wa Mashindano hayo, Massoud Mutiva amesema mashindano hayo ni endelevu na kuwaomba Wachezaji kucheza kwa amani na michuano hiyo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.