FEDHA ZA KODI KUIMARISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO.

YUSSUF JUMA MWENDA

Mamlaka ya Mapato Zanzibar Z. R. A imewataka Wafanyabiashara kuwa na imani na Fedha wanazolipa kupitia Kodi mbali mbali kuwa zinawarejea Wananchi kupitia shughuli za maendeleo.

Akizungumza katika uwasilishaji wa Matokeo ya utafiti juu ya mambo yanayoweza kuongeza Mapato huko Hoteli ya Marumaru Forodhani, Kamishna wa ZRA Yussuf Juma Mwenda, amesema ni vyema kufahamu kuwa Kodi ni sehemu ya kuimarisha huduma za Jamii ikiwemo Maji, Afya na Barabara.

Meneja Mradi kutoka Taasisi ya Kodi ya Norway CMI, Profesa Odd Helge Fjeldstad, amesema njia nzuri ya kuwahamasisha Wananchi kulipa Kodi kwa hiyari ni kuwepo usawa na uwazi kwa walipa Kodi wote, pamoja na kuwa na mbinu za kuwafanya Wafanya Biashara kuwa Marafiki.

Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar chamber of comerse, amao wameendesha utafiti huo, samiha zahor, amesema ukosefu wa elimu ya matumizi ya mifumo umekuwa ukisababisha malalamiko ya Kodi kwa Wafanyabiashara, hivyo watashirikiana na ZRA ili kuona wanawajengea uelewa.

Mtafiti Mwandamizi Lucas Katera amesema utafiti uliangalia maoni zaidi Mashirikiano kwa Sekta ya Umma na Taasisi Binafsi na kushauri kuziwezesha Taasisi Binafsi ili kufanya kazi kwa pamoja.

standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.