Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhakikisha wanawasimamia vyema Wavuvi waliopewa boti na vizimba ili kuhakikisha wanatumia zana hizo kwa matumizi sahihi ili kusaidia ukuaji wa sekta ya uvuvi na kupunguza uvuvi haramu.
Rais Samia amesema hayo Jijini Mwanza katika uzinduzi wa ugawaji wa vizimba 222 vya kufugia Samaki na boti za kisasa 55 kwa Wavuvi kanda ya Ziwa wenye kauli mbiu uchumi wa buluu ni fursa muhimu kwa Wananchi.
Waziri wa mifugo na uvuvi Ndg.Abadalah Ulega amesema Wizara imeweka mkakati wa kuongeza boti hizo hadi kufikia 500 ili zana hizo zifanye kazi ipasavyo itakayosaidia kupunguza uvuvi haramu katika Ziwa Victoria.
Chrisant mtenya ni mmoja kati ya wanufaika wa vizimba ameishukuru serikali kuwagawia vizimba na kuomba viwepo viwanda vya kutengeneza chakula cha samaki.
Ndg.Bakari kadabi ni Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya uvuvi Ziwa Victoria amesema boti hizo za kisasa zitawawezesha Wavuvi kuondokana na uvuvi haramu.
Sekta ya uvuvi inachangia pato la taifa kwa asilimia 1.8 baada ya kuimarishwa katika sekta hiyo pato hilo linatatajiwa kuongezeka hafi kufikia asilimia 10