CHINA KUTOA UFADHILI WA FANI YA VIUMBE WA BAHARINI KWA WAZANZIBARI

RAIS DK.MWINYI NA WAGENI KUTOKA CHINA

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Mhe. Sun Shuxian na ujumbe wake.

   Dkt Mwinyi amefanya mazungumzo hayo Ikulu Mjini Zanzibar na kuishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuisadia Zanzibar katika Sekta mbali mbali ambayo imeifanya kuwa na maendeleo.

   Katika hatua nyengine Dkt. Mwinyi amesema China na Zanzibar zitatiliana saini hati ya ushirikiano katika Sekta ya Uchumi wa Buluu ikiwemo Sayansi na Teknolojia ya Baharini, Uchunguzi wa mazingira ya Bahari, utabiri wa ufuatiliaji na tahtmini ya maafa, pamoja na ulinzi wa mfumo wa ikolojia wa Baharini.

   Naibu Waziri wa maliasili wa China Mhe. Sun Shuxian ameeleza kuwa China inatoa fursa za ufadhili wa masomo kwa Wanafunzi wa Kizanzibari katika fani ya bahari na viumbe wa baharini hivyo amehimiza Wanafunzi kuchangamkia fursa hiyo.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.