Mkuu wa Jeshi la kujenga Uchumi (JKU), Kanal Makame Abdallah Daima, amewataka Wafanyakazi wa Jeshi hilo kufanyakazi kwa bidii na Ufanisi, kwa lengo la kuisaidia Serikali katika kuimarisha Uchumi.
Mkuu huyo wa JKU ameyasema hayo Chuo cha Uongozi JKU Dunga wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Jeshi hilo kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo ikiwa ni muendelezo wa kukumbushana kuhimizana Majukumu yao ya Kazi ya kila siku ndani ya Jeshi hilo.
Mkurugenzi Wakala wa Ulinzi JKU Luteni Kanal Kona Shaame Hamad na Meja Halima Khamis Khatib, amesema ukumbusho walioupata kutoka kwa Wakufunzi wao, utawasaidia kuwajibika vyema katika utendaji wa Kazi wanazozifanya ndani ya Jeshi la kujenga Uchumi (JKU).
stories
standard