SERIKALI SMT YAAGIZA KUPEWA MATIBABU BURE KIJANA MARTIN JOSEPH

MSAADA
English

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga  kwa niaba ya Mhe.Waziri Mkuu dkt.Mwigulu Nchemba  amekabidhi kiti mwendo  kwa kijana mwenye ulemavu Martin Joseph mkazi wa Babati,baada ya familia ya kijana huyo kuomba msaada kwa waziri mkuu alipokuwa kwenye ziara yake mwezi  machi /2026 mkoani humo.

Akizungumza baada ya kukabidhi kiti mwendo hicho Sendiga  amewataka wazazi wa kijana huyo  kukitunza  na kuhakikisha wanampeleka  kwenye matibabu kwa kuwa Serikali imetoa barua maalum ya  msamaha wa matibabu  kwa kijana huyo.

kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara dkt.Andrew Method  amesema kupitia mpango wa bima ya afya kwa wote kijana huyo atapatiwa kadi ya matibabu katika utaratibu wa watu wenye ulemavu.

Aidha  mama mzazi  wa kijana   huyo Anastazia  Sulle ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais dkt.Samia Suluhu Hassan  kwa kupatiwa  msaada huo.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.