Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Wakuu wapya wa Wilaya Watano aliowateua hivi karibuni Ikulu Zanzibar ili kuimarisha Uongozi na uwajibikaji katika utekelezaji wa Sera na mipango ya Serikali
Zikiwa zimepita Siku Mbili tangu Uteuzi huo kutangazwa, mapema leo Viongozi hao wapya wamekula kiapo cha uaminifu, wakiahidi kuitumikia Nchi kwa weledi, uadilifu na kuzingatia sheria na taratibu za Nchi.
Mara baada ya kula kiapo cha uaminifu na kutunza siri za Serikali, baadhi ya Wakuu Wilaya wakaweka wazi mikakati yao ikiwemo kuwaletea maendeleo Wananchi
Katika Uteuzi huo wa Wakuu wa Wilaya Tano, Nafasi Tatu zimechukuliwa na Wanawake na wamesema wako tayari kuvunja vikwazo na kuleta mageuzi chanya, wakisisitiza kuwa Uongozi bora hauangalii jinsia bali uwezo, dhamira na uthubutu.
Katika hafla hiyo Viongozi mbalimbali walishuhudia Uapisho huo ambapo Laila Burhan Ngozi Ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharib 'a' kabla ya nafasi hiyo alikuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa , Riziki Danniel Yusuf Ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'a' , Zuhura Mgeni Othman Ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake , Dkt.Said Haji Mrisho Ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini , Ali Abdallah Natepe Ameapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharib 'b' na hii ndio safu mpya ya Uongozi wa Dkt.Mwinyi katika Ngazi za Wilaya
